kipi kipya?

Maonyesho ya sakiti iliyosasishwa

Katika kivinjari cha Tor Sakiti ya Torkwa kila kichupo chako kinaweza kupatikana kwenye onyesho la sakiti. Hadi wakati wa toleo hili onyesho la sakiti kwenye paneli ya maelezo ya tovuti - kumaanisha kwamba utahitaji kubofya ikoni ya kufuli (au ikoni ya onion ikiwa ni tovuti za onion) iliyo upande wa kushoto wa upau wa anwani ili kuifikia. Washiriki wa kupima utumiaji mara nyingi walitatizika kupata onyesho la sakiti walipoulizwa na watumiaji kwa ujumla walihitaji kufundishwa mahali lilipoishi.

Ili kurekebisha hili, tumehamisha onyesho la sakiti nyuma ya ikoni mpya ya rangi ambayo inakaa kando ya kufuli. Kwa kuongeza, rilei sasa zina flag kusaidia kurahisisha maeneo yao kutambuliwa katika mtazamo; muundo wa nyaya za tovuti za onion umefanywa kwa ufupi zaidi; SecureDrop watumiaji wanaotembelea jina onion linaloweza kusomeka na binadamu sasa wanaweza kuona na kurudi kwenye anwani ya msingi ya onion V3; na paneli kwa ujumla imejengwa upya kutoka mwanzo kwa upatanifu bora na visoma skrini.

Picha ya skrini ya onyesho la sakiti iliyosasishwa ya securedrop.org katika Kivinjari cha Tor kwa kompyuta ya mezani

ikoni mpya ya tovuti ya onion

Hapo awali, tovuti za onion ziliwakilishwa na onion-glyph – a tiny, toleo sawasawa cha nembo ya onion ya Kivinjari cha Tor. Sasa, unapotembelea tovuti ya onion kwenye kivinjari cha Tor 12.5 kwenye kompyuta ya mezani au Android utatambua jambo jipya.

Ni muhimu kutambua huduma za onion si maalum kwa Kivinjari cha Tor na ni bidhaa kwa haki zao zenyewe. Kwa vile kukubaliwa kwa huduma ya onion kumeongezeka miongoni mwa mashirika ya kiraia, mashirika ya haki za binadamu, na vyombo vya habari hata pia msaada kwa huduma za onion kutembelewa na programu za wahusika wengine. Leo,kwa kuongeza Kivinjari cha Tor, unaweza pia kufikia huduma za onion katika programu zinazolingana kama vile Orbot, Kivinjari cha Onion na Brave, kutaja chache. Kwa kuzingatia hilo, haina maana tena kuendelea kuwakilisha tovuti za onion zilizo na ikoni inayohusishwa kwa karibu sana na Kivinjari cha Tor na tunafurahi kutambulisha utambulisho wao mpya leo.

 Picha ya skrini ya tovuti ya onion ya ProPublica kwenye Kivinjari cha Tor kwa kompyuta ya mezani na Android

Uzoefu wa muunganisho ulioboreshwa

Katika Kivinjari cha Tor 10.5 kwenye kompyuta ya mezanitulistaafu Kizinduzi cha Tor kwa kupendelea kiolesura kipya kinachoruhusu watumiaji kuunganishwa na Tor kutoka kwa window ya kivinjari yenyewe. Kipengele hiki kilifungua manufaa yaliyoongezwa ya kuweza kufikia menyu nyingine za Kivinjari cha Tor ukiwa nje ya mtandao ikiwa ni pamoja na mipangilio ya Muunganisho ambayo inatoa utendakazi mkubwa zaidi kuliko ukurasa sawa wa mipangilio wa Kizinduzi cha Tor.

Tangu toleo hilo, washiriki wa majaribio ya utumiaji wakati mwingine wamekuwa na ugumu wa kujua jinsi ya kuunganisha baada ya kutoka kwa kichupo cha Unganisha hadi Tor. Ili kurekebisha hili tumefanya kitufe cha Unganisha kupatikana katika upau wa anwani wa ukurasa wowote unaotembelea ukiwa nje ya mtandao na Kivinjari cha Tor kitaunganishwa kiotomatiki baada ya kusanidi kiungo katika mipangilio ya Muunganisho. Pia tumeboresha mwonekano wa hali ya muunganisho wa kivinjari ambayo sasa inaweza kupatikana katika sehemu ya juu kulia ya window ya kivinjari na utaona ikoni mpya ya muunganisho ikitokea kwenye kivinjari kote pia.

Picha ya skrini ya kichupo cha mipangilio ya Muunganisho kabla ya kuunganisha kwenye Kivinjari cha Tor cha eneo-kazi

Ufikikaji bora

Kwa vile Kivinjari cha Tor kinategemea Utoaji Uliopanuliwa wa Usaidizi wa Firefox, tunatumia tena uzoefu wa mtumiaji wa mwisho wa Firefox kadiri tuwezavyo ili tuweze kuelekeza rasilimali zetu kwenye masuala ya faragha na usalama. Hata hivyo, Kivinjari cha Tor pia hujumuisha kurasa nyingi maalum na vipengele juu ya Firefox.

Sambamba na juhudi za muda mrefu za Mozilla ili kuboresha ufikivu wa Firefox, tulianza ukaguzi wetu wa ufikivu ili kuandika masuala na Kivinjari cha Tor kwa vipengele maalum vya kompyuta ya mezani. Uhakiki huu sasa umekamilika, na tunaanza kupeleka marekebisho ya kwanza katika ambayo itakuwa juhudi za matoleo mengi ili kuboresha ufikiaji wa Kivinjari cha Tor.

Tangu Kivinjari cha Tor 11.5 tumeweka upya vipengee kadhaa ikiwa ni pamoja na vibandiko vya kubadilisha vifurushi (kuhusu:tbupdate), onyesho la sakiti, paneli ya kiwango cha usalama, vidadisi mbalimbali na sehemu nyingine za kromu ya kivinjari. Ikiwa unatumia kisoma skrini au teknolojia nyingine yoyote ya kusaidia, tungependa kupata msaada wako kupima marekebisho ya zamani na ya baadaye nakujitolea kama mhariri wa alpha na kutoa maoni kwa watengenezaji wetu juu ya jukwaa la Tor.

Picha ya skrini ya logi ya mabadiliko ya ndani na paneli ya kiwango cha usalama kilichopanuliwa kwenye Kivinjari cha Tor ya mezani

Usaidizi wa lugha ya Kifini

Katika Kivinjari cha Tor 12.0 tuliongeza msaada kwa Kialbania na Kiukreni. Sasa, kutokana na kazi nzuri ya watafsiri waliojitolea na washirika wetu katika Maabara ya Ujanibishajitunayo furaha kujumuisha Kifini (Suomi) kama chaguo la lugha kwenye kompyuta za mezani na Android pia. Ukiona hitilafu katika Kifini au lugha nyingine yoyote, unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kuchangia katika tafsiri ya Tor Browser, nyaraka zake na tovuti zetu kwenye tovuti yetu. lango la ujanibishaji.

Picha ya skrini ya ukurasa wa muunganisho katika Kifini katika Kivinjari cha Tor cha kompyuta ya mezani na Android

tuma mrejesho yako

Ikiwa una mapendekezo juu ya jinsi tunavyoweza kuboresha toleo hili, tafadhali tujulishe. Asante kwa timu zote katika Tor, na kwa wale wengi waliojitolea, ambao wamechangia kwa toleo hili.

Unaitaji msaada?

Angalia FAQ katika jamii yetu

Tembelea Msaada

Wasiliana

wasiliana na sisi moja kwa moja!

Jiunge nasi kwenye IRC